Habari Mpya :

Habari Mpya

KAMBI TIBA YA GSM FOUNDATION YAMALIZA KAZI PWANI, YAELEKEA TANGA

Imeandikwa na Henry Mdimu on Thursday, September 15, 2016 | 10:42

Na Mwandishi Wetu
Wazazi nchini wametakiwa kuwa na moyo wa kujali afya za watoto wao hasa zinapotokea fursa za tiba za bure kwenye jamii zao kwani ni nadra sana kwa fursa hizi kujitokeza katika jamii za kitanzania. 
Hayo yamesemwa na mbunge wa Chalinze Mhehimiwa Ridhwani Kikwete alipotembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwana vichwa vikubwa na mgongo wazi. 
Huu ni mkoa wa 10 kwa kambi hii kutembelea, huku ukiwa ni msimu wa tatu wa kambi tiba hizi zenye lento la kuokoa miasma ya watoto takriban 3500 wanaohisiwa kupoteza maisha kila mwaka köa mujibu wa tafiti za MOI za mwaka 2002, ambazo zinasema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka lakeni ni 500 tu huweza kufika kwenye tiba huku changamoto kubwa ikitajwa kuwa ni uchache wa madaktarim ba ukubwa wa gharama za tiba. 
Awamu ya kwanza ya kambi tiba ya GSM ilipita mikoa ya Mwanza, Shinyanga. Singida, Dodoma na Morogoro. Ya pili ikapita Mtwara, Songea, Mbeya na iringa. Hii awamu ya tatu itapita katika mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Mara.
PICHANI JUU: Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi, Dk Aggey Geoffey(Wa pili kutoka kushoto), na Dk Silas Msangi( Wa kwanza kushoto), mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha. Kulia ni Afisa uhusiano wa GSM Foundation Khalphan Kiwamba. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Kibaha - Pwani Bi. Chiku mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha - Pwani. Kutoka kulia ni Mkurugeni Mkuu wa GSM Foundation, Shanon na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Tumbi - Kibaha Bw. Dk Aggrey Geoffrey
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na madaktari waliokuwa wakihusika na kuandikisha watoto waliokuwa wakifanyiwa upasuaji.
Mzazi akiwa na mwanae aliyefanyiwa upasuaji.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa nusu Kaputi, Bw. Ogutu Ogonga mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha - Pwani. Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwashukuru waganga waliotoka GSM Foundation kwa moyo wao wa pekee wa kujitolea kuwafanyia upasuaji watoto hao.
Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi, Dk Aggrey Geoffreyakitoa mrejesho juu upasuaji uliofanyika hospitalini hapo.
Afisa Habari wa GSM Foundation Bw Khalphan Kiwamba akitoa maelezo juu ya upasuaji ulivyofanyika katika Hospitali ya Tumbi - Kibaha. Wanaomsikiliza kutoka kushoto kwenda kulia ni Shannon Kiwamba, Munge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete na Kaimu Mganga Mkuu Aggrey Geoffrey
Wageni wakiohuduria mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mtaalamu wa nusu Kaputi, Bw. Ogutu Ogonga mara baada ya kumaliza zoezi la kukagua kambi hiyo.

HABARI PICHA: MCHUNGAJI DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AKIHUDUMU NCHINI MAREKANI.

Imeandikwa na Henry Mdimu on Monday, August 22, 2016 | 17:58

Na Mwandishi Wetu
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani) yuko nchini Marekani kwa huduma ya kiroho tangu jumanne iliyopita Agost 16,2016 ambapo alianza kuhudumu ijumaa Agost 19,2016 katika Kanisa la "Assemblies Of God Agape Church" lililopo Boston Marekani.

Huduma ya Mchungaji Dkt.Kulola inaendelea katika majimbo mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Dallas, Texas, Houston na Arizona.

Aidha Mchungaji Kulola ametoa shukurani zake za dhati kwa familia yake, Kanisa la EAGT Lumala Mpya, ndugu, jamaa pamoja na marafiki kwa kuendelea kumuombea kwa huduma anayoifanya nchini Marekani ambapo watu wengi wanaokoka na kuponywa.
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akihudumu nchini Marekani.
Picha ya pamoja baada ya huduma katika jimbo la Boston
Mchungaji Kulola (katikati) na familia yake
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola(kulia).
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATENDAJI WA IDARA YA MAZINGIRA PIA AHUDHURIA MSIBA WA SHAKILA SAID

Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  amekutana na kufanya mkutano wa kazi na watendaji wa ofisi yake ya Idara ya Mazingira kujadili kwa kina namna ya kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika leo, Ikulu, Dar es salaam ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, Makamu wa Rais ameawaagiza watendaji wa idara hiyo waache kukaa ofisini na badala yake waende kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema hali ya uharibifu wa mazingira ikiachwa iendelee kama ilivyo inaweza ikasababisha madhara makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwamo wataalam wa mazingira na wadau wa maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na tatizo hilo.

Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira na kuonya wataobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.

Baadhi ya watendaji waliotoa taarifa kuhusu hali ya mazingira nchini wamekiri kuwa hali ya uharibifu wa mazingira siyo nzuri hasa kwenye mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Manyara, Geita, Singida na Kilimanjaro.

Inakadiriwa kuwa takribani hekta 400,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka hali ambayo inapelekea baadhi ya wanyama kutoweka.

Watendaji hao wameiomba serikali iongeze bajeti ya kutosha ili waweze kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi.

Makamu wa Rais ametumia siku ya mapumziko ili kujadiliana na kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini. Mkutano huo wa kazi unaendelea tena hapo kesho.

PICHANI JUU: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira, kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu Oisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka Abduwakil Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi Idra ya Mazingira Bi. Esther Makwaia akiwasilisha taarifa ya hali ya Mazingira nchini kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira mara baada ya kupata taarifa za maendeleo, mipango na mikakati ya Idara hiyo, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwenye mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kuwasili msibani kwa Bi. Shakila, Mbagala Chalambe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombelezo ya msiba wa marehemu Shakila Said.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu wa marehemu Shakila nyumbani kwa marehemu Mbagala Chalambe.
 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Bi. Shakila Said
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza jambo na Issa Muhidin Michuzi kwenye msiba wa Bi. Shakila.
 Swala ya maalum kabla ya kwenda kuzika
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akishiriki dua maalum ya kumuombea Marehemu Shakila Said ambaye alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa Taarab nchini.
Mwili wa Marehemu ukipelekwa makaburini tayari kwa maziko.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUISAIDIA SEKTA YA MAJI NCHINI

Imeandikwa na Henry Mdimu on Thursday, August 18, 2016 | 19:25

Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO).

Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi.

Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.

“Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji” alisema Bi. Bird

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.

“Changamoto ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo” alisema Mhandisi Luhemeja.

Benki ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo, pamoja na Uchumi na Biashara.

PICHANI JUU: Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam.
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WAKADIRIAJI MAJENGO AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.


Amesema serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.


Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.

PICHANI JUU: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
 Rais wa  Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
 Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SBL yatangaza kudhamini elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa mara nyingine imetangaza mpango wa kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha.

Huu ni mwaka wa sita mfululizo ambapo SBL inatoa msaada kwa wanafunzi wa ndani wanaochukua kozi za shahada katika vyuo vikuu vya Tanzania chini ya programu ya kampuni ijulikanayo kama “Skills for Life”. Jumla ya wanafunzi 31wa Tanzania tayari wameshanufaika na mpango huu ambao ni sehemu ya Mfuko wa Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL Foundation).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha fomu za maombi kwa ajili ya udhamini zinapatikana katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza au kupitia tovuti ya www.eablfoundation.com.

Wanyancha amesema mpango huo uko wazi kwa wanafunzi kutoka nchi nzima ya Tanzania ambao ambao tayari wamepata usajili wa kujiunga na vyuo vikuu nchini katika fani za Biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Uhandisi na Sayansi ya Chakula katika ngazi ya shahada kutoka vyuo vikuu hapa nchini.

Mfuko wa EABL ulianza kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi kuanzia wanaojiunga na vyuo vikuu mwaka 2005 ambapo hadi sasa zaidi ya wanafunzi 238 wamenufaika kwa mpango huo wakiwemo 31 kutoka Tanzania. Wengi walionufaika tayari walishamaliza masomo yao na wanafanyakazi katika makampuni mbalimbali katika ukanda huo. Mpango huu upo katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mfuko wa EABL umetumia jumla ya zaidi ya Tshs billion 5 kuugharamia tangu mwaka wa 2005. 

Udhamini huu hugharamia ada ya masomo, vitabu, malazi, fedha za kujikimu na programu za ushauri kwa waombaji watakaofanikiwa.

“Lengo letu kuu kupitia mpango huu ni kuwawezesha waombaji kutimiza ndoto zao maisha,” alisema Wanyancha na kuongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Septemba 20, 2016.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini kuchangamkia fursa hiyo ili kwa kutuma maombi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ujao.

MAHITAJI MUHIMU: Fomu za maombi zilizojazwa vizuri zikiwa zimeambatanishwa na barua ya usajili kutoka kwa taasisi ya elimu ya juu, udhibitisho wa hitaji la kifedha na nakala za vyeti vya elimu ya sekondari kidato cha nne na cha sita.

PICHANI JUU: Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha ( kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) Wakati wa kutangaza mpango kampuni hiyo wa kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha.Pembeni yake ni Meneja wa Miradi ya Jamii wa SBL Hawa Ladha katika mkutano uliofanyika mapema leo katika ofisi za SBL,Temeke jijini Dar es salaam.
Meneja wa Miradi ya Jamii Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza mpango wa kampuni hiyo kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha,kulia kwake ni Mkurungezi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za SBL zilizopo Temeke Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo mapema leo asubuhi katika ofisi za SBL zilizopo Temeke jijini Dar es salaam.

Msimu wa pili wa kambi tiba ya GSM Foundation wafungwa rasmi Iringa, maisha ya watoto 37 yaokolewa

Na Mwandishi Wetu
Kambi tiba ya GSM iliyokuwa imeingia katika msimu wake wa pili tangu Agosti mosi mwaka huu, imefungwa rasmi mkoani Iringa, huku watoto 37 wakiwa wamefanyiwa upasuaji, na wengine zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji, huku suala la uimara wa afya likiwa kipaumbele cha kwanza.

Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002, unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.

Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa vichwa vikubwa na vikubwa  na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.

Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa mingine.

Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona,

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amewaomba GSM Foundation warudi tena iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto waliomo mkoani humo.

Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.

PICHANI JUU: Msemaji wa GSM Foundation, Khalfan Kiwamba `Kiwadinho',(Kulia) akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Meneja wa Meneja wa Taasisi hiyo Shannon Kiwamba(Wa kwanza kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Robert Salim(wa Pili kutoka kushoto, na Kibwana Matukio kutoka GSM Foundation(Mwenye Miwani).
, Mkuu wa Mkoa wa iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Dk Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto).

UNA HABARI? Kambi tiba ya GSM Foundation meshaanza kazi mkoani Iringa

Imeandikwa na Henry Mdimu on Wednesday, August 17, 2016 | 16:12

Na Mwandishi Wetu
Kambi tiba inayoendeshwa na Taasisi ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili kwa ufadhili wa GSM Foundation inayojaribu kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi leo imeanza kazi Mkoani Iringa, huu ukiwa ni mkoa wa nne tangu msimu wa pili wa ziara yake ya kuzunguka nchi nzima kuanza.

Kaimu mkuu wa kambi tioba hiyo, Daktari Bingwa Hamis Shaaban(Pichani juu) kutoka MOI ameiambia Millardayo.com kwamba kumekuwa na hamasa ndogo kwa wazazi kuleta watoto wao kwa ajili ya tiba hii ya bure katika msimu huu, ukilinganisha na msimu wa kwanza ambapo jumla ya watoto 101 walifanyiwa upasuaji,

Katika awamu hii ya pili, mpaka leo hii ni watoto 35 wamefanyiwa, huku ukiwa ni mkoa wa mwisho kwa kambi hii kupita, hali inayoleta ukweli kwamba inaweza kumalizika bila kufikia lengo la kutibu watoto 100 na zaidi kama ilivyokuwa awamu ya kwanza.

Afisa habari wa GSM Foundation, Bw Khalphan Kiwamba, `Kiwadinho', amesema sababu kuu ni wagonjwa kuwa mbali na eneo ambapo tiba inafanyika, na kambi haikuweza kusogea zaidi kwa sababu za kiufundi kwani upasuaji wa watoto hawa unahitaji maabara za kisasa ambazo zinapatikana katika Hospitali za mikoa tu.

Kiwamba kwa upande wake amewaomba wakazi wa iringa kujitahidi kupashana habari ili watoto wengi wapate kupata tiba hii iliyofadhiliwa tayari,

Kambi tiba ya GSM kwa msimu huu wa pili inamalizika Agosti 18 mwaka huu wa 2016, ambapo baada ya tathmini, tarehe za msimu wa tatu zitatangazwa.
 Mmoja kati ya watoto waliohudhuria kambi tiba ya GSM ya msimu wa pili akikaguliwa na daktari
Wataalam wakiendelea na kazi ya tiba maabara

HABARI ZA BURUDANI

habari nyinginezo »

HABARI ZA KITAIFA

Habari nyinginezo »

MAKALA

habari nyinginezo »

HABARI ZA KIMATAIFA

habari nyinginezo »

HABARI ZA BIASHARA

Habari nyinginezo »
 
BLOG DESIGNERS : Bongoclan Blog Besigners | Anga Designers | Call us 0752184797
Copyright © 2011. Mdimu's Blog - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Blogger